Phil Foden Ampa Rodri Maua Yake

Phil Foden kiungo wa klabu ya Manchester City amempa maua kiungo mwezake wa klabu hiyo Rodri baada ya mchezo wao wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Aston Villa.

Kiungo Phil Foden raia wa kimataifa wa Uingereza amemua kumpa sifa kiungo huyo mwenzake raia wa kimataifa wa Hispania kutokana na kiwango ambacho amekua akikionesha ndani ya klabu hiyo hivi karibuni.phil foden“Nakosa mpaka cha kusema Rodri anafanya kila kitu, Sioni udhaifu wowote kwenye mchezo wake nafikiri ni mchezaji wetu muhimu zaidi kwa upande wangu, Lakini pia kwa upande wangu naona ni kiungo bora wa chini duniani asilimia 100 kwakua anafanya kila kitu”Alisema winga huyo wa kimataifa wa Uingereza.

Kiungo Rodri na winga Phil Foden ni wachezaji waliohusika kwenye mabao yote manne ambayo Manchester City walifunga kwenye ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Aston Villa, Ambapo Rodri alifunga bao moja na kupiga pasi moja ya bao huku Phil yeye akifunga mabao matatu.phil fodenKiungo Rodri amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu ya Manchester City tangu msimu uliomalizika jambo ambalo limemfanya mpaka mchezaji mwenzake kumsifia hadharani, Lakini pia kiungo huyo anashikilia rekodi mpaka sasa akiwa hajapoteza michezo 63 akiwa uwanjani ndani ya kikosi cha Man City.

 

Acha ujumbe