Phil foden amefanikiwa kuvunja rekodi ya Lionel Messi baada ya kufunga katika mchezo wa derby ya Manchester leo mapema katika dimba la Etihad.

phil fodenPhil Foden anakua mchezaji mdogo zaidi wa kwanza kufunga magoli 50 kwenye timu anayofundisha Pep Guardiola baada ya kufunga leo akiwa na umri wa miaka 22 na siku 127 huku Lionel Messi yeye alifikisha magoli hayo akiwa na miaka 22 na siku 164 wakati huo akiwa chini ya Pep katika klabu ya Fc Barcelona.

Hivo kinda huyo wa kiingereza anakua ndio kinara kwasasa katika vijana ambao wamewahi kufunga mabao 50 chini ya mwalimu huyo, kitu chqa kukumbuka pia ni kua Messi akishaichezea Barcelona kwa misimu minne kabla Pep hajachukua timu mwaka 2008/09 huku Foden yeye akicheza chini ya kocha huyo tu.

Phil Foden toka alipopewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza na mwalimu Pep Guardiola amekua na kiwango bora sana na kukiendeleza kiwango hicho huku akifanikiwa kuchukua tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwenye ligi hiyo mara mbili mfululizo.

phil fodenKiungo huyo wa kiingereza amefanikiwa kutakata leo katika mchezo wa Deby baada ya kufunga magoli matatu sawa na mshambuliaji matata wa klabu hiyo Earling Haaland.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa