Philippe Coutinho hana nia ya kuondoka Barcelona licha ya uvumi unaoendelea kumhusisha na kuhamia mahali pengine, hii ni kwa mujibu wa wakala wa Mbrazili.

Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool – ambaye alitumia msimu uliopita kwa mkopo huko Bayern Munich – alipewa nafasi ya kurudi Ligi Kuu msimu wote wa joto baada ya kuhangaika kurejea kwenye fomu yake Camp Nou.

Wakati dili la kurejea England likikwama kutimia, amejikuta tena akitupiwa jicho na kugonga vichwa vya habari, na ripoti nchini Italia zinadai kwamba Juventus iko tayari kumsajili mchezaji huyo wa miaka 28.

Philipe Coutinho

Hata hivyo, wakala wa Coutinho, Kia Joorabchian amekanusha mpango wa uhamisho kupitia Mundo Deportivo: “Sijasikia chochote na hatuna mpango wa uhamisho kutoka Barça, na ndio Coutinho anaweza kuchangia mafanikio msimu huu.”

Licha ya jeraha la msuli wa hivi karibuni, staa huyu anafurahia nafasi yake kikosi cha kwanza huko Camp Nou tangia Ronald Koeman alipochukua hatamu, akifunga mabao mawili na asisti mbili tayari msimu huu katika mashindano yote.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili anajivunia jumla ya mabao 23 katika mechi 84 tangu alipowasili Catalonia kutoka Liverpool mnamo 2018, na Coutinho aliingia mkataba na Barca hadi 2023.


 

FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Coutinho, Philippe Coutinho Hana Mpango wa Kuondoka Barcelona, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa