Ipi hukumu kubwa zaidi kuwahi kutolewa duniani? Hakuna anayejua jibu sahihi. Ila ipo moja tunayoweza kuitumia kama mfano, japo sina hakika kama ndiyo hukumu ya kikatili zaidi kuwahi kutolewa katika historia ya dunia, ila inafaa kuwa mfano mzuri. Ni ile ya Pontio Pilato kutoka mji wa Judea kwenda kwa Massih Issa Bin Mariam.
Watu walipompeleka nabii Issa mikononi mwake wakitaka auwawe, alisikiliza mashitaka kutoka pande zote mbili. Hakuona kosa linalomkabili nabii Issa kustahili kufa, ila kwa kuhofia kiti chake cha uongozi, alipitisha hukumu ya kifo kama walivotaka wale washitaki. Kumradhi, kama sijasimulia ipasavyo.
Kila nikiifikiria hii habari, kichwani mwangu ananijia muitaliano Perluigi Collina. Yes, referee bora wa mwaka wa FIFA mara sita. Referee bora kuwahi kutokea katika historia ya soka. Referee pekee ambaye hadi anastaafu halaumiwi na timu yoyote kuwa aliwahi kuwaonea.
Subiri kwanza, hapa namzungumzia mtu aliyeongeza dakika 3 katika fainali ya UEFA mwaka 1999 pale Camp Nou, Manchester United wakasawazisha na kupata bao la ushindi mbele ya Bayern Munich. Collina ni mtu asiyetingwishwa.
Labda ujasiri wa maamuzi yake ulitokana na maisha aliyokulia utotoni. Si rahisi kulelewa na mama Mwalimu na baba askari alafu usiwe mtu wa sheria. Asingetetereka maamuzi hata mbele ya akina Duncan Ferguson. Angetenga tuta akiwa anacheka halafu ukimlalamikia anakutwanga kadi akikukaripia. Yule ndiyo Perluigi Collina.
Usidhani alikuwa hivo kwa wachezaji tu, hata waamuzi wenzake walikoma kumtambua. Kabla ya mechi angewaweka wasaidizi wake chini, awape ‘tution’ ya namna timu zote zinavocheza na wachezaji wakuwaangalia kwa jicho la tatu. Ndiyo maana Ronaldo De Lima alijiamini vile mbele ya wajerumani pale Korea Kusini katika fainali ya kombe la dunia 2002.
Marehemu Steve Jobs alisema, “Njia pekee ya kufanikiwa ni kupenda unachofanya”. Nadhani ndiyo maana Collina amefanikiwa. Immagine aliacha kazi ya jeshi na shahada yake ya uchumi ili akawe muamuzi.
Drops and Wins!
Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.



warda
Namkubaligi sana pierluigi#Meridianbettz
JULIANA
Asante kwataharifa
Zeiyana
Pierluigi ni refaa mwenye mbinu yingi na hufanyaji wake wa kazi
Magdalena
rfa yupo vizuri sana na akiwa katika kazi zake apendagi masihara wala hana upendeleo yupo makini na kazi zake
Lydia Emmanuel Magoti
Namkubali Sana uyo Collina akiwaga kwenye kaz anaga masiala anafanya vile kinavyo fanywa kitekelezwe kipasavyo
felister
ni refa mwenye mbinu nyingi
Sadick
Refa mahiri kuwahi kutokea duniani, wakati wake hakuhitaji VAR na maamuzi yake yalikuwa sahihi 100%#meridianbettz
Samira
Ni kweli kabisa sura sio roho
Ester jackson
Daah asante kwa nakala nzuri
Ernest
Collina Amejizolea umaarufu mkubwa sana hasa kwa style yake ya uamuzi maana alikuwa imara sana na watu walitokea kumpenda kupita maelezo
Janeflora malisa
Yupo sawa
Mwajumah
Pierluig ni refa mwenyew mbinu nyingi namkubali sana#Meridianbettz
Caroline
Kweli kabisa sura si roho
Nasra
Yupo vzuri sana
Dorophina
Collina ni refa wa kiwango kizuri sana na alikuwa anatenda haki kwa wote hakika ni refa bora hajakaa tokea
Asia Abdy
Yuko vizur sana
Khadija
Asante kwa makala nzuri#meridianbettz
Hope mwaikuka
Refa wang namba 1
Sabrina
Mareferee kama Collina wange kuwepo kipindi hichi VAR isingekua na kazi.
Saupha mohamed
Yupo vizuri
Furahav
Yuko poa sana.
Issa
Collina referee mwenye uwezo mkubwa sana asiekiwa na skendo zozote kwenye soka toka kipindi hiko
Devotha
Asante kwa taarifa
Gabriel
Collina amechukua umaarufu sana katika kuchezesha kombe la dunia pia ni kocha ambaye yuko makin na wachezaji wajanja ambao wanajiangusha bila sababu namkubal sana 👍 huyu refa
Shafii
Siku zote ukipenda kile unachokifanya katika maisha yako basi ni rahisi Sana kufanikiwa.
Omary lukumbi
Ila ana sura tata sana
Sauda
Yuko poa kabisa.
aisha
Refa mwenye kipaji chake
Amiri Kayera
Refaree mweny viwang vyak
Johnmary joel
Yupo sahihi namkubali sana#meridianbett
Povel
Noma sana hiiiii
David Pere
Collina Amejizolea umaarufu mkubwa sana hasa kwa style yake ya uamuzi maana alikuwa imara sana na watu walitokea kumpenda kupita maelezo