Kocha mkuu wa AC Milan Stefano Pioli amesikitishwa na washambuliaji wake kwa kupoteza nafasi nyingi mbele ya lango huku msururu wao wa kupoteza mechi katika Serie A ukiisha kwa kuchapwa mabao 2-1 na Napoli Jumapili.

 

Pioli Achukizwa na Washambuliaji Wake

 

Matteo Politano aliiweka Napoli mbele kwa bao la mkwaju wa penati baada ya Sergino Dest kumfanyia madhambi Khvicha Kvratatskhelia. Nae Olivier Giroud aliisawazishia Milan dakika ya 69 lakini, Giovanni Simeone akafunga kwa kichwa dakika ya 78 na kuhakikisha Napoli inarejea kileleni mwa Serie A.

“Sijaridhika hata kidogo na pia wachezaji wangu hawapaswi kuridhika,” Aliiambia DAZN. “Tulifunga bao moja tu, ambalo halikutosha kwa yote tuliyounda, “Natumaini tutajifunza kutokana na hili kuwa wabunifu zaidi mbele ya lango kwasababu tulifanya kila kitu sawa isipokuwa kwa  makosa na ukosefu wa uamuzi katika maeneo yote mawili ya adhabu.”

 

Pioli Achukizwa na Washambuliaji Wake

Pioli alisema kuwa ni vigumu kuilaumu safu yake ya ulinzi wakati Napoli ndiyo timu pekee iliyopata nafasi hiyo ya kuifunga AC Milan pia ana uchungu zaidi kwa kukosa nafasi ambazo walibadilisha. Milan baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza msimu imeshuka hadi nafasi ya tano na  itasafiri kuelekea Empoli ambapo watakipiga Octoba 1 baada ya mapumziko ya Kimataifa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa