Beki kisiki na wa muda mrefu wa Barcelona, Gerald Pique amedai kuwa klabu pekee anayotamani kucheza na kustaafu ni Barcelona na hana mpango wa kwenda timu nyingine yoyote endapo kocha Koeman atamfukuza.

Beki huyo wa kati alieleza yaliyopo moyoni mwake wakati wa kipindi cha the Twitch na kuweka wazi kuwa anataka kusalia Barcelona.

“Siku ambayo naacha kuchezea Barcelona, itakuwa ndio siku naacha mpira. Sitocheza timu nyingine yoyote. Kuna wachezaji wanahama kwa ajili ya pesa na sababu nyingine, lakini mimi kama kesho Koeman akinambia niondoke, nitaondoka”, alieleza Pique.

“Kukosolewa ni sehemu ya mpira na lazima tuzikubali”. Alimalizia beki huyo.

Alipoulizwa kuhusu kuja kuchukua nafasi ya urais wa timu hiyo hapo baadae Gerald Pique alidai kuwa hicho ni kitu ambacho kinamfurahisha hasa kwa ukweli kuwa Barcelona ni timu yake lakini ni mapema sana kuelezea jambo hilo.

Barcelona huenda wakawatoa wachezaji kadhaa majira haya ya joto, ingawa jina la Gerald halijatajwa lakini mchezaji huyu anaweza kubadili mkataba wake ili kusaidia klabu kiuchumi.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa