Beki wa Barcelona, Gerard Pique,33 atakuwa nje kwa kipindi cha miezi minne ijayo kutokana na jeraha baya la goti alilolipata wakati wa mchuano wa Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) dhidi ya Atletico Madrid waliowapiga 1-0 mnamo Novemba 21, 2020.

Madaktari wamefanya tathmini yao na kutuarifu kwamba Pique atalazimika kuwa nje kwa takriban miezi minne ijayo kuuguza jeraha baya la goti,” akasema kocha Ronald Koeman kwa kusisitiza kwamba tukio hilo ni pigo kubwa kwa safu ya ulinzi kambini mwa Barcelona.

 

pique, Pique Nje Miezi 4 Baada ya Uchunguzi., Meridianbet
Gerard Pique Akitolewa nje baada ya kuumia.

Ushindi wa 1-0 ambao ulisajiliwa na Atletico dhidi ya Barcelona uliwapaisha hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa jedwali la La Liga kwa alama 20, moja nyuma ya viongozi Real Sociedad.

Kwa upande wao, Barcelona ambao walipoteza mchuano wao wa tatu kati ya mechi nane zilizopita walisalia katika nafasi ya 11 kwa alama 11 sawa na Valencia na Osasuna.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

22 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa