Pliskova Atemwa Nje French Open

Michuano ya French Open inaendelea kupamba moto huku baadhi ya mastaa wakijipata wanatolewa baada ya kuruhusu kichapo kwenye michuano hii.

Karolina Pliskova ameshindwa kutoboa kwenye raundi ya tatu na kuruhusu kichapo kutoka kwa bingwa namba 31 wa dunia Petra Martic kwenye raundi ya tatu ya michuano hii. Mwanadada huyu ambaye pia aliingia nusu fainali mwaka 2017, ameshindwa kuvuka raundi ya 3 kwa miaka 2 katika michuano hii French Open.

Pliskova alikuwa kwenye fomu nzuri na kufanikiwa kumchapa bingwa namba moja wa Uingereza Johanna Konta kwenye Italian Open kule Roma mwezi uliopita.

Baada ya kumshinda Pliskova, Martic ambaye alifikia raundi ya 4 mwaka 2012, anatarajia kukutana na Kaia Kanepi kutoka Estonia ambaye ameshawahi kucheza robo fainali mara 2 au Mrusi Veronika Kudermetova anayeshika nafasi ya 68 duniani.

3 Komentara

    Asante meridianbet #kwa taarifa

    Jibu

    Hoo!pole wala usikate tamaa songa mbele#meridianbettz

    Jibu

    Gud news

    Jibu

Acha ujumbe