Kocha wa zamani wa klabu ya PSG na Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino inaelezwa aliiktataa ofa ya klabu ya OGC Nice ambayo walimpatia hivi karibuni ili kujiunga na klabu hiyo.

Kocha huyo ambaye aliachana na na klabu ya PSG mwishoni mwa msimu uliomalizika baada ya klabu hiyo kuajiri mwalimu mpya klabuni hapo kutoka klabu ya Lile.

pochettinoPochettino ameonesha kutokua na mpango wa kuchukua kazi hiyo ambayo amepewa na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa na kusubiri kazi nyingine ambayo inaweza kuja siku za mbeleni.

Siku chache zilizopita rais wa klabu ya Nice alizungumza kua hawajamuhitaji kocha huyo na hawana mpango nae lakini taarifa za ndani zinaeleza klabu hiyo ilipelekea ofa kumuhitaji kocha raia wa Argentina huku yeye ndo akiikataa ofa huyo.

Mauricio inaaminika anaamini anaweza kupata kibarua kwenye timu kubwa siku za mbeleni ambapo anaamini ndio timu ya hadhi yake na kuweza kukua pia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa