Klabu ya PSG inapanga kufanya mapinduzi makubwa katika uongozi wa timu hiyo na wamepanga kuvunja mkataba wa meneja wa timu hiyo Mauricio Pochettino.

Paris Saint-Germain wana mwelekeo wa kumfukuza Mauricio Pochettino siku zijazo, wakisubiri mkutano wa mwisho kufanyika mara baada ya Raisi wa klabu hiyo Al Khelaifi kurejea kutoka Qatar.

Kocha wa Roma, Jose Mourinho na kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane wanatajwa kuchukua nafasi ya Pochettino pale PSG lakini mpaka sasa hakunaaliyethibitisha taarifa hizo.

 

pochettino, Pochettino Akalia Kuti Kavu PSG., Meridianbet
Leonardo – Mkurugenzi wa Michezo wa Paris Saint-Germain

Taarifa za ndani zinasema mkurugenzi wa michezo Leonardo ataondoka pia ndani ya klabu hiyo na tayari timu imeshapewa taarifa huku nafasi yake ikichukuliwa na Luis Campos.

Luis Campos atatangazwa kama mkurugenzi mpya na mshauri wa rais baada ya mikutano miwili chanya huko Doha na Al Khelaifi, makubaliano sasa yamekamilika na kufungwa, atatangazwa rasmi hivi karibuni.

Wachezaji wengi pia wataondoka PSG msimu huu wa joto, Aurelién Tchouaméni yumo kwenye orodha ya muda mrefu lakini Real Madrid wanaongoza kwenye mbio hizo na sasa wanakaribia kumsajili kiungo huyo Mfaransa.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa