Kocha wa klabu ya Chelsea Mauricio Pochettino ameonesha kusikitishwa na majeraha ambayo ameyapata mchezaji wake raia wa kimataifa wa Ubelgiji Romeo Lavia.
Pochettino wakati akiongea na wanahabari leo amesema “Ni kipindi kigumu kwakweli amecheza dakika 30 tu tangu ajiunge na sisi,Pindi klabu imemsajili kutoka Southampton na alionesha kua tayari lakini alianza kusumbuliwa na mguu”Kutokana na kauli ya kocha huyo inaonesha kwa kiwango kikubwa sio mchezaji tu ambaye atakua anaumia, Lakini pia benchi la ufundi kwa ujumla unasikitishwa na hali ambayo anakutana nayo kiungo Romeo Lavia kwasasa.
Kiungo Romeo Lavia amekua akipitia wakati mgumu sana tangu ajiunge na klabu ya Chelsea katika majira ya joto yaliyopita, Kwani alijiunga akiwa na majeraha akitokea Southampton baada ya kupona amepata majeraha mengine tena.Kiungo Romeo Lavia atakosa sehemu ya msimu iliyobaki kutokana na majeraha ambayo alishayaeleza kocha Mauricio Pochettino, Ni wazi mchezaji huyo atarejea tena msimu ujao ikiwa msimu mbaya sana kwa upande wake kwani amefanikiwa kucheza dakika 30 tu tangu ajiunge na Chelsea.