Mauricio Pochettino alikiri kuwa timu yake iliachwa na uchovu baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Brighton kwenye Ligi ya kuu ya EPL.
Wenyeji walianza mchezo vyema kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, wakiwa mbele kwa mabao 2-0 kwa mabao ya Enzo Fernandez na Levi Colwill.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Lakini Brighton walipiga bao kupitia kwa Facundo Buonanotte, kabla ya Conor Gallagher kutolewa nje kwa kadi nyekundu hadi kipindi cha kwanza.
Chelsea ya wachezaji 10 walifanya vya kutosha katika kipindi cha pili, hata hivyo, huku Fernandez akifunga kwa mkwaju wa penalti na kuendeleza uongozi wao hadi Joao Pedro dakika za lala salama.
Pochettino alisema: “Ni ligi yenye ushindani zaidi. Tulianza vizuri, tulikuwa tunacheza vizuri 11 vs 11. Ilikuwa kipindi kigumu cha pili baada ya kuwa pungufu mchezaji mmoja. Brighton ni timu nzuri sana na inacheza vizuri, ilibidi tuingie ndani lakini tulifunga bao la tatu “
Timu imechoka, sote tumechoka, lakini kwa ujumla tuna furaha. Baada ya Newcastle, tulihitaji kuonyesha sura tofauti. Ndiyo maana nina furaha. Alisema Pochettino.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Kuhusu kadi nyekundu ya Gallagher na matumizi ya VAR wakati wa mchezo, aliongeza kuwa haamini ilikuwa nyekundu anahitaji kuiiona tena. Wanaelewa waamuzi lakini wanahitaji kuwaelewa pia.
Kwa nini walitoa penalti na kisha kuangalia VAR kwa mpira wa mikono wa Colwill? Ni vigumu kuelewa kwa nini. Sio kulalamika, kukosoa. Kwa nini penati ya Mudryk ilikuwa ikingoja VAR na akatoa mpira wa mikono? Inashangaza sana jinsi tunavyotumia VAR wakati mwingine. Alihoji kocha huyo wa zamani wa PSG.