Klabu ya Tottenham tayari inafanya mazungumzo ya kumrejesha tena meneja wao wa zamani Mauricio Pochettino, ambaye kwa sasa anahudumu kama meneja kule Paris Saint-Germain.
Kwa mujibu wa Skysport, Tottenham wamefikiria na wameanza jitihada za kumrejesha Pochettino Spurs.
Ni miezi 18 tangia Muargentina huyo aondoke Spurs, akifanikiwa kuanza vyema kama meneja wa PSG ambako pia alisaini mkataba wa mda mfupi wa miezi 18.

Akiwa Ligue 1 Pochettino tayari ameshashinda mataji mawili ya ndani Ufaransa, alifanikiwa pia kuwafikisha PSG kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuwachapa Barcelona na Bayern Munich, lakini wakachapwa na Manchester City.
Hata hivyo, Pochettino hajaficha ukweli kuwa anatarajia kurejea Spurs ambako bado anaamini ana biashara ambayo haijakamilika huko. Lakini ni wachache ambao walitarajia angerejea mapema hivi.
Kwa kuzingatia umuhimu na mchango wake mkubwa klabuni hapo, Spurs wanaweza kufanikiwa kumrejesha meneja wao, japokuwa hii inaweza kuwa gharama tofauti na angekuwa hana mkataba na klabu nyingine.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Kila la kheri kwake
Karibu sana