Pochettino: Nipo Hapa Kushinda

Kocha wa klabu ya Chelsea Mauricio Pochettino ameweka wazi kua sera na utamaduni wa klabu hiyo ni kushinda mataji na yeye mwenyewe yupo ndani ya timu hiyo kwajili ya kushinda.

Pochettino amesema unapokua ndani ya klabu ya Chelsea ambayo historia yake imejengwa kwa ushindi unapaswa kushinda, Lakini kama utashindwa kushinda basi ni jambo ambalo sio zuri.pochettinoAkizungumza na wanahabari kocha huyo wa zamani wa klabu ya Tottenham ameweka wazi kua ndani ya Chelsea lengo kubwa ni kuhakikisha wanashinda michezo yao, Lakini kama watashindwa kushinda michezo yao basi ni wazi watakua wamekwama kwa namna moja ama nyingine.

Kocha huyo pia amegusia suala la kua na kikosi kichanga kwa maana ya timu ambayo imeundwa na vijana wengi, Akieleza kua wanapaswa kukua taratibu kwani ni ngumu kuwalaumu vijana hao kwakua bado wamekosa ukomavu.pochettinoHaikuishia hapo ambapo Pochettino pia aliendelea kusikitishwa na majeraha ambayo yamekua yakiindama timu yake, Ameeleza ni ngumu sana kwa klabu kufanya vizuri wakati ambapo timu yako inaandamwa na majeraha haswa wachezaji wako muhimu.

Acha ujumbe