Kiungo wa Manchester United Paul Pogba (28) amekataa ofa ya kusaini mkataba mpya na klabu hiyo wenye thamani ya £50m ambao ungemfanya alipwe kiasi cha £350,000 kwa wiki.
Imeelezwa kuwa Pogba amesimamia msimamo wake wa kutaka kuondoka klabuni hapo mara baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu akiwa mchezaji huru kama watashindwa kumuuza katika kipindi hiki cha usajili.
PSG wameonyesha nia ya kuhitaji huduma yake kwa dau la £43m lakini Manchester United wamemtaka mchezaji huyo kusalia mpaka atakapo maliza mkataba wake.
Je, United wako sawa kumuacha aondoke bure msimu ujao au wachague kufanya biashara kipindi hiki ?
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!
Ernest
Wakati wa Pogba kutamba sasa sababu anajuwa kipindi cha nyuma alidharaulika sana kutoka kwenye uongozi wa Man U adi kwa Mashabiki, Soon mambo yatakuwa hivi hivi kwa De Gea