Watoto wa mjini wanasemaga “top in town” kwa maana ya kitu kinachoteka vichwa vya habari. Paul Pogba ndio habari ya Manchester United kwa misimu kadhaa sasa.

Kila dirisha la usajili, Pogba atahusishwa na kuondoka United. Kama sio mchezaji moja kwa moja, basi wakala wake, Mino Raiola lazima atawekwa kwenye lensi za wanahabari. Paul ndio habari ya mjini.

Akiwa amebakiza miezi 5 tu kwenye mkataba wake na United, kwa hali ilivyo kiuhalisia, Paul ni mchezaji huru ifikapo Juni 30,2022. Anamkataba mpya mezani lakini, hajausaini mpaka sasa ikiwa ni miezi imepita toka apewe mkataba huo.

Rangnick

Ujio wa Ralf Rangnick na kazi anayoifanya kocha huyo ndani na nje ya uwanja, vinatajwa kumvutia Paul na, kunauwezekano mchezaji huyo akaamua kubaki United na kusaini mkataba mpya na The Red Devils.

Hii ni baada ya Ralf kumuonesha Paul imani na kumueleza bayana maono na mipango yake kwa mchezaji huyo na klabu kwa ujumla. Hii inamfanya kiungo huyo kujifikiria mara mbili kabla hajaamua kuondoka/kusaini mkataba mpya. Endapo Ralf atapatiwa kazi ya kuiongoza United kama kocha mkuu wa muda mrefu, kunauwezekano tukamuona Pogba ndani ya uzi wa United msimu ujao.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa