Pogba Amkingia Kifua Ole Solskjaer

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amejitokeza na kumtetea kocha wake Ole Gunnar Solskjaer kutoka kwenye kejeli za Mourinho kuhusu malezi.

Pogba anadai kuwa Mourinho ni mtu ambaye anapenda kupingana na wachezaji muda wote na huamua kuwatenga bila sababu yoyote, tofauti na kocha wake wa sasa Ole Solskjaer ambaye ana maelewano mazuri na wachezaji na hata kama ataweka benchi wachezaji fulani anatambua uwepo wao.

Mourinho alimfundisha Paul mwaka 2017 na akaisaidia United kuchukua kombe la ligi na kombe la Europa League.

Paul anasema kwamba yeye na Mourinho walikuwa wanaelewana sana mpaka pale iliposhindikana. Na mpaka kesho hawezi kusema kilitokea nini kati yao. Mourinho amekuwa akihusishwa na tabia za kupenda kuwakomoa wachezaji ambao hawafuati matakwa yake.

“Ole ni wa tofauti sana na hawezi kupingana na wachezaji kama Mourinho… Ole anaweza asikuchague kwenye mechi lakini anatambua uwepo wako, tofauti na Mourinho. Na hiyo ndiyo tofauti yao kubwa” Aliandika Pogba kwenye post yake ya tweeter.

Maneno hayo yalikuja siku kadhaa baada ya kejeli za kurushiana maneno kati ya Ole na Mourinho ambayo yalitokana na kujiangusha kwa Son kwenye mechi kati ya Tottenham na Man United, ambapo Man united walishinda 3-1.

Mourinho alionekana kumkejeli Ole kutokana na kumsema sana Son ambaye alidai kufanyiwa faulo na Mc Tominay katika mechi hiyo, kitendo ambacho kilipelekea kufutwa kwa goli la Cavani.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

5 Komentara

    Paul yupo sahihi

    Jibu

    Poul yupo makini

    Jibu

    Mourinho inabidi ajiangaliye kwa sababu sio picha nzuri kwa wachezaji

    Jibu

    Pogba yupo sahihi ole ni kocha mzuri sana

    Jibu

    Binadam hatupo sawa

    Jibu

Acha ujumbe