Pogba hajahusishwa na kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kwenye mechi tangu aliporejea kutoka kwa jukumu la kimataifa mapema mwezi huu.

Ole Gunnar Solskjaer anasema uimara wa kikosi chake unampa shida za kuchagua wachezaji kila wiki, lakini Paul Pogba hatahusika katika maamuzi yake wikendi hii wakati kiungo huyo anaendelea kuwekwa benchi kwa sababu ya jeraha.

paul pogba

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alicheza mara tatu wakati wa mapumziko ya kimataifa lakini hajawahi kuichezea United katika moja ya michezo yao miwili tangu alipata jeraha, ambalo meneja Solskjaer alisema alilipata wakati akiichezea nchi yake.

Raia huyo wa Norway alithibitisha kwamba kiungo huyo ana jeraha la kifundo cha mguu, lakini ni tofauti na jeraha ambalo lilimfanya awe nje kwa mechi nyingi za kampeni iliyopita.

Hata hivyo, Solsjaer ana furaha na kikosi chake anaamini kuwa kiko fiti na ana uwanja mpana wa kufanya maamuzi. Anatumaini ataondoka na ushindi wikiendi hii dhidi ya Southampton.


 

USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa