Kimsingi, Paul Pogba anahesabu siku tu kabla mkataba wake na Manchester United kuisha muda wake. Kituo kinachofuata baada ya Old Trafford ni kipi?

Pogba ambaye kwa sasa anauguza majeruhi ya mguu, hatarajiwi kuonekana tena uwanjani akiwa amevaa jezi ya United. Hii inatokana na uhalisia kuwa, kiungo huyo ataondoka klabuni hapo baada ya mkataba wake wa miaka 5 kuisha mwishoni mwa msimu huu.

Kocha wa muda wa United, Ralf Rangnick amethibitisha kuondoka kwa Paul kwa kile alichosema kuwa, hamuoni mchezaji huyo, kocha mpya (Erik Ten Hag) wala uongozi wa United ukitaka kusaini mkataba mpya kuendelea kuwepo Old Trafford.

Licha ya kuwepo kwa taarifa za United kumpatia Paul ofa ya mkataba mpya toka mwaka jana, mchezaji huyo hajafanya chochote kwenye ofa hiyo – hajaikubali wala kuikataa. Ipo kama alivyopewa, wala United hawajaongeza au kupunguza chochote kwenye ofa hiyo waliyoitoa toka awali.

Pogba, Pogba, Kituo Kinachofuata Ni?, Meridianbet

Juventus, PSG, Barcelona na Real Madrid zinahusishwa na Pogba ambaye, mpaka wakati huu, hajafanya maamuzi yeyote kuhusu timu atakayojiunga nayo baada ya kuondoka Manchester United mwishoni mwa msimu huu.

Kwa muda wa miaka 5 aliyokaa United, mahusiano ya kiungo huyu na mashabiki wa klabu hiyo yamekua yakibadilika kila kukicha. Mchezo dhidi ya Norwich pale Old Trafford, ulitoa taswira ya kipekee baada ya mashabiki kumzomea mchezaji huyo wakati anafanyiwa mabadiliko kwenye mchezo huo.

Pogba, Pogba, Kituo Kinachofuata Ni?, Meridianbet

Hali hiyo iliendelea kwenye mchezo dhidi ya Liverpool licha ya mchezaji huyo kuwepo uwanjani kwa dakika 5 tu kabla ya kutoka kwa majeruhi ya mguu. Kama mchezo dhidi ya Liverpool ndio ulikua wa mwisho kwake, basi Paul Pogba anaondoka United akiwa hana mahusiano mazuri na mashabiki wa klabu hiyo ambayo inataabika msimu huu.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa