Pogba Kufanya Mazoezi Carrington

Kiungo wa zamani wa klabu ya Juventus Paul Pogba anatarajiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu ya Manchester United huku akiwa anasubiri kupata timu mpya ambayo ataitumikia baada ya kumalizana na Juventus.

Kiungo Paul Pogba ambaye amekaa nje ya uwanja kwa takribani mwaka mzima akituhumiwa kujihusisha na utumizi wa dawa za kuongeza nguvu michezoni alifanikiwa kurshinda rufaa yake na kuruhusiwa kurejea uwanjani, Lakini klabu yake ya Juventus iliamua kumvunjia mkataba ili akatafute timu nyingine kwa wakati huu.pogbaKufuatia kuvunjiwa mkataba na klabu ya Juventus kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa inaelezwa atakua kwenye uwanja wa mazoezi wa Man United akijifua wakati anasubiri timu, Jambo hili limeibua mitazamo tofauti tofauti kwani baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wakitamani kumuona akivaa jezi ya klabu hiyo tena huku wengine wakisema hapaswi kupewa nafasi nyingine ya kuitumikia klabu hiyo.

Ikumbukwe kiungo Paul Pogba alikua akiitumikia klabu ya Manchester United kwa kipindi cha miaka saba kabla ya kutimkia Juventus, Hivo kiungo huyo anaweza kufikiriwa na benchio la ufundi la klabu ya Man United kama akionesha ubora na huenda akapewa mkataba wa kuitumikia timu hiyo ambayo ipo chini ya kocha mpya Ruben Amorim.

Acha ujumbe