Baada ya hali ya sintofahamu kwa muda, Ralf Rangnick amethibitisha kuondoka kwa Paul Pogba mwishoni mwa msimu huu.

Katika mahojiano ya takribani dakika 15 na waandishi wa habari, Rangnick amethibitisha kuwa, (kwa hali ilivyosasa hivi), haionekani kama Pogba atasaini mkataba mpya na Manchester United. Na sio Paul tu, anadhani hata uongozi wa klabu na Erik Ten Hag pia, hawanampango wa kusaini mkataba mpya na mchezaji huyo.

Pamoja na kutosaini mkataba mpya na kuondoka kama mchezaji huru, Rangnick ameonesha kutofurahishwa kwake na namna ambavyo Paul amekuwa akiitumikia Man United kwa muda wote aliokuwepo klabuni hapo. Kwa Ralf, ni suala la kushangaza kumuona mchezaji huyo akiitumikia Timu ya Taifa (Ufaransa) kwa nguvu na ari kubwa lakini, anapokuwa kwenye jezi ya Man U, hafanyi lolote linalofanana na hilo.

Pogba, Pogba Kuondoka Manchester United., Meridianbet

Ametolea mfano wa mchezo uliopita dhidi ya Liverpool ambapo, kwa jicho na uchambuzi wake kama kocha, goli la kwanza walilofungwa United ni matokeo ya utendaji usio na tija uwanjani ambao Pogba aliufanya na hivyo kuigharimu timu muda mfupi na kisha kuomba kutolewa nje kwa majeruhi.

Kwa taarifa hii ya Ralf Rangnick, ni rasmi kuwa dakika 5 za mchezo dhidi ya Liverpool ndio mara ya mwisho kumuona Paul akiwa kwenye jezi ya United hasa wakati huu ambao atakua nje ya uwanja kwa takribani wiki 4 akiuguza majeraha ya mguu.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa