Pogba Afunguka Kuwa Aliwai Kuwa na Msongo wa Mawazo

Kiungo wa klabu ya Man United Paul Pogba ameweka wazi kuwa alishawa kupambana na msongo wa mawazo kwenye kipindi akiwa chini ya kocha wa kireno Jose Mourinho.

Mshindi wa kombe la dunia ambaye alishawai kuwa mchezaji ghali wa dunia kwenye kipindi ambacho alisainiwa kwa mara ya pili akitokea Juventus mwaka  2016.

Paul Pogba amekuwa akikosolewa sana kwenye kipindi ambacho amekuwa kwenye klabu ya Man Utd kutokana na kuwa na kiwango ambacho kimekuwa cha kupanda na kushuka, mshindi huyo wa kombe la dunia hajashinda kombe lolote kubwa tangu mwaka 2017 kombe la Europa League na EFL Cup.

Paul akizungumza na La Figaro akiwa kwenye majukumu ya kimataifa na timu ya taifa ya Ufaransa, Pogba ametoa siri kuwa alikuwa anapambana na maswala yake binafsi akiwa uwanjani.

“Nilikuwa na msongo wa mawazo kwenye kazi yangu, lakini hatuwezi kuzungumza hili. Muda mwingine huwezi jua, muda mwingine unataka ujitenge, kuwa peke yako, hizi ni ishara mbaya”

Pogba anasema alianza kuanza kupambana na hali hiyo akiwa chini ya Jose Mourinho akiwa kama kocha wake, Hili lilianza kipindi nikiwa chini ya Jose Mourinho.

“Unajiuliza maswali mwenye, unashangaa ikiwa kama kuna kosa ulifanya sababu hukuwai kupitia hali hiyo kwenye maisha yako. Wachezaji wakubwa wote wanapitia hii hali kwa kipindi furani, lakini wachache wanazungumzia hili.

“Msongo wa mawazo hauepukiki, utahisi kuwa mwili, kichwa na inaweza kwenda mpaka mwezi mzima hata mwaka, ukiwa hauko sawa. Lakini huwezi sema hili kwenye popote.

“Tunapata pesa nyingi sana na kiukweli hatulalamiki, lakini hili halikuzuii kupitia vipindi vigumu kuliko wengine, kama wengine kwenye maisha.

“kwasababu unatengeneza pesa nyingi, ndio utakuwa na furaha? sio kama hivyo kwenye maisha, lakini kwenye mpira wa miguu, hili halitupiti, sisi sio watu wenye uwezo wa ajabu, lakini ni binadamu kama wengine.”


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe