Mchezaji nyota wa klabu ya Juventus Paul Pogba ambaye alipaswa kufayiwa upasuaji siku ya leo jijini Lyon nchini Ufaransa umeahirishwa mpaka siku ya kesho kwa sababu ya kupata uthibitisho ikiwa atakosekana kwenye michuano ya kombe la dunia.

Pogba alipata majeraha ya goti akiwa nchini Marekani kwenye michezo ya Pre-season, na awali ilibidi afanyiwe upasuaji nchini Marekani kabla ya klabu hiyo kuamua kumtafutia mshauri wa afya wa kuangalia ni namna gani atafannyiwa upasuaji ili aweze pona haraka.

Pogba, Pogba Upasuaji Wake Kuahirishwa, Meridianbet

Pogba leo alitarajiwa kukutana na mshauri leo jijini Lyon, lakini kuna taarifa zimetoka kuwa leo ilishindikana kukutana naye na imeahirishwa na imependekezwa wakutane kesho.

Pogba ana machaguzi mawili kwenye upasuaji wake, moja aondoe sehemu ya “meniscus” ambapo atakuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili, au kutibu kidonda ambacho kiko ndani ya goti na tiba hii itachukua muda mrefu kupona, hii itiba inaweza kumpelekea kukosa michezo ya kombe la dunia.

Klabu ya Juventus inahitaji kujua ni muda gani atakuwanje ya uwanja ili waweze kuendelea kwenye soko la usajiri na mpaka Sergej Milinkovic-Savic  ndio anaoneka mbada wa kuziba nafasi hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa