Ikiwa imesalia siku moja Kikosi cha Simba kuvaana na Yanga, Jeshi Polisi Kanda Maalumu ya Dar, kwa kushirikiana na vyombo vingine vhya ulinzi na usalama limejipanga kuimarisha ulinzi katika mchezo huo wa watani wa jadi.
Akizungumza na waandishi wa habari, mapema leo Kamanda wa Polisi, Lazaro Mambosasa, amesema: “Tumejipanga kuimarisha ulinzi kwa kuweka askari wa kutosha katika maeneo yote yanayozunguka Uwanja wa Mkapa na barabara zinazoingia na kutoka uwanjani hapo kuhakikisha hakutokei vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa amani.”amesema Kamanda Mambosasa
“Tunatoa wito kwa mashabiki na wapenzi wa soka kufika uwanjani mapema ili kuepusha msongamano wakati wa kuingia uwanjani hapo kwani milango ya uwanja itafunguliwa mapema na ulinzi wa polisi utakuwepo wa kutosha,” amesema.
“Mashabiki waepuke kuingia na chupa za maji majukwaani, kuingia na silaha ya aina yoyote, kupaki magari ndani ya uwanja pasipokuwa na kibali maalum pamoja na kukaa sehemu ambazo tiketi zao haziruhusu,” amesisitiza Kamanda Mambosasa.
TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO
Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!
Simba bingwa tuu
Yanga kesho msituangushe
Simba ladhima tuwapige utopolo goli3-0
Watakuwa wamefanya Jambo jema
Watani wa jadi mambo yanazidi kunoga
Simba sikuzote awezi kushuka kilelen
Simba bingwa
Simba bingwa
Kesho patachimbika kwa mkapa
Safi kamat ya ulinzi
Simba baba lao