Klabu ya Chelsea imemtambulisha rasmi Graham Potter kama kocha wake mkuu ambapo amesaini mkataba wa miaka 5 kukinoa kikosi hicho. Potter amesajiliwa Chelsea baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu ambao Thomas Tuchel alikuwa nao.

 

Potter Atambulishwa Chelsea

Potter ambaye ni raia wa Uingereza ameingia darajani hapo jana akitoka katika klabu ya Brighton ambayo imekuwa ni klabu inayofanya vizuri msimu huu kutokana na jinsi ambavyo wachezaji wanacheza na yeye akiwa ni mwalimu wa timu hiyo.

Kocha huyo toka msimu huu uanze akiwa na Brighton ndani ya mechi sita ameshinda michezo minne, sare moja na kapoteza mchezo mmoja ambao ni dhidi ya Fulham. Mechi ya kwanza ya Graham itakuwa ni dhidi ya Fulham hapo kesho ambapo atakuwa ugenini majira ya saa nane na nusu.

 

Potter Atambulishwa Chelsea

Chelsea mpaka sasa katika msimamo wa EPL ndani ya mechi sita imeshinda mechi tatu, sare moja na kupoteza mechi mbili na mpaka sasa yupo nafasi ya sita. Chelsea ilihitaji mabadiliko ya haraka sana kutokana na kuwepo presha kwa bodi na kila kitu kutokana na kuwa ni timu ambayo imeongoza kutumia pesa nyingi kwenye usajili hivyo matokeo hayaridhishi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa