Kocha mkuu wa klabu ya Chelsea Graham Potter ausifia ubora wa Conor Gallagher ambae aliipatia timu hiyo alama 3 siku ya Jumamosi baada ya kufunga bao dakika 90 la uongozi wa bao 2-1.
Chelsea ilikuwa ugenini ikicheza dhidi ya Crystal Palace, na Gallagher alicheza kwa mkopo msimu uliopita timu hiyo. Ilikuwa ni ushindi wa kwanza wa Potter toka ajiunge na timu hiyo huku mechi yake ya kwanza akitoa sare ambayo ilikuwa ni ya RB Salzburg kwenye klabu bingwa. Potter alisema;
“Ninampenda sana Conor. Ni mtoto mzuri sana na anatamani sana kufanya vyema, kuichezea klabu hii, kuwa na mafanikio katika Chelsea”.
“Natumai ni mwanzo tu wa maisha yenye mafanikio makubwa Chelsea kwa Conor Gallagher”.
Chelsea mpaka sasa wapo katika nafasi ya 5 baada ya michezo saba akiwa na pointi 15, huku akiwa amepoteza michezo miwili na tetesi zikisema kuwa wanakaribia kukamilisha usajili wa Christopher Nkunku aje kuongeza nguvu klabuni hapo.
Potter na vijana wake mechi inayofuata watacheza dhidi ya AC Milan kwenye michuano ya Klabu Bingwa huku wakiwa hawajashinda hata mechi yao moja kwenye michuano hiyo.