Kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea na Brighton Hove and Albion Graham Potter anatajwa kama mbadala wa kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag ambaye anaonekana kua na wakati mgumu klabuni hapo kwasasa.
Kocha Potter hana timu toka alipoondolewa kwenye klabu ya Chelsea mapema mwaka huu, Hivo wamiliki wa klabu hiyo anamuona kama mtu sahihi wa kumrithi Erik Ten Hag.Anaetarajiwa kua mmiliki wa hisa aslimia 25 klabuni hapo Sir Jim Ratcliffe inaelezwa ndio anafanya mazungumzo na kocha huyo wa zamani wa Uingereza ili aje avae viatu vya Mdachi Erik Ten Hag.
Kocha Erik Ten Hag mpaka sasa anaonekana kukalia kuti kavu katika klabu hiyo kwani mpaka sasa wameshatupwa nje kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya,Tena wakiwa wanashika mkia na kwenye ligi kuu muenendo hauridhishi.Kocha Graham Potter ndio anaongoza kwenye orodha ya makocha wanaotajwa kumrithi Ten Hag klabuni hapo, Huku Sir Jim Ratcliffe akielezwa ndio anasukuma zaidi jambo hilo kutokea na hii ni baada ya kumalizika kwa mchakato wa yeye kununua hisa zake klabuni hapo.