Premier League na FA wamethibitisha kuwa michezo yote ya wikiendi hii imeahirishwa kutokana na maombolezo ya msiba wa malkia wa Uingereza Elizabeth II.

Waraka wa Premier League: “Kwenye kikao cha asubui ya leo, vilabu vya ligi kuu ya Uingereza vitatoa heshima kwa mtukufu malkia  Elizabeth II. Kutoa heshima kwa ajiri ya maisha yake na mchango wake kwenye taifa, na kama alama ya heshima, wikiendi hii michezo ya Premier League yote itahairishwa, ikiwemo ya jumatatu jioni.”

Richard Masters, Mkurugenzi mtendaji wa Premier League alisema: “Sisi na vilabu vyetu tungependa kutoa heshima kwa mtukufu Malkia kwa huduma yake isiyo na kikomo kwa nchi yetu.

“Kama kiongozi aliyehudumu kwa muda mrefu, amekuwa kivutio kwa wengi na ameacha urithi kufuaitia maisha yake aliyoyaishi. Hiki ni kipindi cha majonzi makubwa sio tu kwa taifa, lakini kwa mamilioni ya watu dunia ambao walivutiwa nae, na tunajumuika kwa pamoja kuomboleza kifo chake.”

Waraka wa FA: “Mtukufu malkia alikuwa mlezi wa chama cha soka na ameacha alama isiyofutika kwenye soka la taifa letu. Kama alama ya heshima kufuatia kifo chake, Chama cha soka Uingereza kimeungana na kufuta michezo ya soka kati 9-11 septemba.

“FA imethibitisha kuahirisha michezo yote ikiwemo Barclays Women Super League, Barclays Women Championship, the Vitality Women FA Cup, na Isuzu FA Trophy, haitachezwa wikiendi hii.

“Pia tunathibitisha kuahirishwa kwa michezo ya National League System [NLS], hatua 1-6, ikiwemo Vanarama National Leagues, Women’s Football Pyramid [WFP], Tiers 3-7, na michezo yote ya ‘grassroots’ nchini Uingereza imeahirishwa.”

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa