Kwa mujibu wa AS, PSG wameanza mazungumzo na wakala wa Cristiano Ronaldo juu ya uwezekano wa kuhama kutoka Juventus msimu huu wa joto.

Mkataba wa Ronaldo unamalizika mnamo Juni 2022, lakini kulingana na ripoti kadhaa nchini Italia, Massimiliano Allegri ametoa ruksa wa kuuzwa kwa staa huyu mwenye miaka 36 ambaye analipwa € 31m kwa mwaka huko Turin.

Chanzo hiki toka Uhispania kinathibitisha kuwa Ronaldo hayuko kwenye mipango ya Allegri kwa msimu ujao, na nyota huyo wa Ureno anatafuta njia ya kusepa dimbani msimu huu wa joto.

Ronaldo Amewambia Wachezaji Wenzake Anataka Kuondoka Juve
 

PSG wameripotiwa kufungua mazungumzo na mwakilishi wa mchezaji huyo Jorge Mendes, lakini mazungumzo na Juventus bado hayajaanza rasmi.

Miamba hawa wa Serie A wako tayari kumuuza Ronaldo kwa takribani €30m, na PSG wanaweza kumtoa Mauro Icardi kwa makubaliano ya kubadilishana.

Kulingana na ripoti hiyo, PSG sio klabu pekee inayopenda kumsajili nyota huyo wa zamani wa Real Madrid kwani Manchester United inafikiria kumleta nyota wao wa zamani pale Old Trafford.

Kwa mujibu wa Tuttosport, Juventus wako tayari kumbadilisha Cristiano Ronaldo na Paul Pogba, lakini Donny van de Beek pia ameibuka kuwa lengo la Juventus, ambao wanahitaji kuimarisha safu yao ya kati.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa