Nchini Ufaransa klabu ya Paris Saint Germain mashabiki wa klabu hiyo waligoma kushangiria na wachezaji wao kwenye mchezo dhidi ya Lens ambao uliisha kwa sare ya 1-1 na kuifanya klabu ya PSG kutawazwa kuwa mabingwa.

Baada ya kutawazwa kuwa mabingwa wa Ligue 1, mashabiki wengi wa klabu ya PSG walitoka nje ya uwanja wa Parc des Princes, na kwenda kushangalia mtaani badala ya kushangilia pamoja na wachezaji wao.

PSG

Hii sio mara ya kwanza kwa mashabiki wa klabu ya PSG kutoka nje ya uwanja na kuwaacha wachezaji uwanjani, kutoka nje ya uwanja ni aina yao ya kufikisha ujumbe kwa wachezaji na uongozi wa klabu, kuwa kuchukua ubingwa wa Ligue 1 pekee haitoshi na wanahitaji kuchukua ubingwa wa Ulaya na makombe mangine makubwa barani humo.

Klabu ya PSG imefanya uwekezaji mkubwa ndani ya kikosi chao ili kuhakikisha wanakuwa na timu bora ambayo inaweza kushindana na vilabu vikubwa ulaya, kwenye msimu wa 2019/20 walifanikiwa kucheza fainali ya ulaya na klabu ya Bayern munich, na kupoteza kwa goli 1, na Bayern Munich kutawazwa kuwa mabingwa wa ulaya.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa