PSG wameweka kipaumbele kwa kumsajili Yan Diomande, mchezaji wa pembeni mwenye umri wa miaka 19 wa RB Leipzig, ambaye amefunga mabao 12 na kutoa asisti 8.

Hata hivyo, ada ya usajili inayotajwa kuzidi €100 milioni imeifanya gharama hiyo kuwa suala linalozua wasiwasi katika mipango ya kocha Luis Enrique.
Wakati huo huo, Bradley Barcola anatarajiwa kufanya mazungumzo na PSG kuhusu mustakabali wake, huku Arsenal FC na Liverpool FC zikionyesha nia ya kumsajili. Inaripotiwa kuwa Barcola anatafuta nafasi zaidi ya kuanza kikosini baada ya kutotumika mara kwa mara katika baadhi ya mechi muhimu chini ya Luis Enrique.
Ripoti pia zinaeleza kuwa P aris hawamuwanii Eli Junior Kroupi, huku wakielekeza nguvu zao kwa Diomande na Maghnes Akliouche. Ada inayotajwa kwa Kroupi kutoka AFC Bournemouth pia inazidi €100 milioni.
Katika hatua nyingine, PSG wako karibu kukamilisha usajili wa kipa kijana wa AC Milan, Alessandro Longoni. Kipa huyo anaweza kuanza kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza hivi karibuni baada ya kutunza clean sheets tano katika mechi 17 za vijana.
PSG pia wamejiunga na Manchester United na Arsenal katika mbio za kumuwania kiungo wa West Ham United, Mateus Fernandes. Hata hivyo, thamani yake inayoripotiwa kufikia pauni milioni 80 inaweza kusababisha ushindani mkubwa wa zabuni.

Mashabiki wa Paris walimpigia kura Khvicha Kvaratskhelia kuwa mchezaji bora wa mwezi Mei baada ya maonyesho yake muhimu, ikiwemo kushinda penalti iliyosababisha bao la kusawazisha katika fainali ya UEFA Champions League. Warren Zaïre-Emery na João Neves pia walitajwa kung’ara katika kipindi hicho.
Baada ya ushindi wa Paris katika fainali uliotokana na penalti iliyokosa kufungwa na Gabriel Magalhães, nahodha Marquinhos alimfariji na kueleza kuwa amekuwa na msimu wa “kipekee” na kwamba alikuwa “beki bora duniani” mwaka huu.
Hatimaye, mashabiki walipiga kura kuchagua bao bora la PSG la mwezi Mei kutoka mechi dhidi ya FC Lorient, Bayern Munich, Stade Brestois 29, RC Lens, Paris FC na Arsenal, huku mabao ya Ousmane Dembélé, Désiré Doué na Mbaye yakiwa miongoni mwa yaliyoingia kwenye orodha ya mwisho.


