Luis Enrique amesisitiza kuwa PSG hawatacheza kwa kujilinda licha ya kuongoza kwa jumla mabao 5-4 dhidi ya Bayern Munich, akitaka timu yake icheze kwa kushambulia katika mchezo wa marudiano kwenye Allianz Arena dhidi ya tishio la Harry Kane.

Warren Zaire-Emery anatarajiwa kuziba nafasi ya beki wa kulia, huku Fabian Ruiz akirejea kikosini na Desiré Doué akipewa nafasi mbele ya Bradley Barcola.
Kikosi kinachotarajiwa pia kinawajumuisha Matvei Safonov, Nuno Mendes, Willian Pacho, Marquinhos, Vitinha, João Neves, Khvicha Kvaratskhelia na Ousmane Dembélé.
Luis Enrique amesema PSG hawatakaa nyuma kulinda matokeo yao, akilenga ushindi mjini Munich. Pia alikumbusha ushindi wa zamani walioupata Munich na kuitaka timu yake kushinda presha ya mashabiki wa Allianz Arena pamoja na ubora wa Kane.
Nahodha wa Arsenal Martin Ødegaard amesema watakutana aidha na PSG au Bayern katika hatua inayofuata, huku PSG wakiwa na faida ya bao moja. Bukayo Saka pia alidokeza kuwa ana mpinzani anayempenda zaidi bila kumtaja.



