Winga wa klabu ya Chelsea raia wa Marekani Christian Pulisic inaelezwa atakua nje ya uwanja kwa miezi kadhaa baada ya kupata majeraha tena.

Winga huyo wa kimataifa wa Marekani amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara ndani ya klabu hiyo tangu ajiunge na timu hiyo akitokea klabu ya Borussia Dortmund. Pulisic ambaye alikua ameanza kua vizuri chini ya mwalimu mpya Graham Potter amepata mejaraha yatakayomueka nje kwa muda wa miezi kadhaa.PulisicKocha wa klabu ya Chelsea Graham Potter wakati aifanya mahojiano na wanahabari siku ya leo ameweka wazi kuhusu majeraha aliyoyapata staa huyo anaweza kua nje ya uwanja kwa miezi kadhaa lakini wanategemea iwe pungu ya hiyo.

Klabu ya Chelsea imekua ikiandamwa na majeraha zaidi msimu huu kwani wachezaji wengi ndani ya kikosi cha kwanza ndani ya klabu hiyo wamekua wakiandamwa na majeraha, Pulisic anaongeza idadi ya wagonjwa ndani ya klabu hiyo ambao watakua nje kwa muda mrefu.PulisicKocha Potter pia amegusia kuhusu majeraha ya Raheem Sterling ambaye yeye ameeleza atakua nje ya uwanja kwa muda pia, Lakini anafikiri mchezaji huyo atarudi uwanjani mapema kuliko staa Christian Pulisic japokua anaeleza bado wanafatilia maendeleo yake.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa