Bingwa wa US Open, Emma Raducanu ameachana na kocha wake Torben Beltz baada ya kuwa pamoja kwa miezi 5.
Raducanu alimuajiri mjerumani huyo ambaye anajulikana kwa kumnoa Angelique Kerber katika taaluma yake lakini ameshindwa kudumu na bingwa huyo wa US Open chini ya mwaka mmoja.
“Nataka nimshukuru Torben kwa kunifundisha, utaalamu na kujitoa kwa zaidi ya nusu mwaka. Ana moyo mkubwa na nimefurahia muungano wetu katika kipindi tulichokuwa pamoja.” alisema Raducanu.
“Nahisi muelekea bora kwaajili ya ukuaji wangu ni kubadili mfumo wa mazoezi, wakati LTA wakinisaidia katika kipindi hichi cha mpito.” aliongeza.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.