Nyota wa klabu ya Manchester City Raheem Sterling yupo jijini London kuweza kukamilisha uhamisho wake wa kwenda klabu ya Chelsea huku akitarijiwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kujumuika na timu hiyo nchini Marekani.
Raheem Sterling muda wowote anatarajiwa kutangazwa kuwa mchezaji wa klabu yachelsea, lakini inabidi akamilishe vipimo vya afya kabla ya kusaini rasmi kuachana na klabu ya Manchester City.
Leo saluni maarufu jijini London imechapisha picha ya Sterling akiwa anatengeneza mtindo mpya wa nywele. Kuonekana kwake London kumetoa mwanga kuwa yuko mbioni kumalizana na chelsea.
Kocha wa klabu ya Chelsea anaamini usajiri wa Sterling utamsaidia kuboresha kikosi chake, hususani kwenye upande wa viuongo washamuliaji wanaotokea upande wapembeni.