Amebakiza michezo 6 ya kuiongoza Manchester United kama kocha wa muda lakini, Ralf Rangnick ni zaidi ya kocha. Anawapasomo vigogo wa klabu hiyo.

Rangnick alikabidhiwa mikoba wa Ole Gunnar Solskjaer kwa mkataba wa miezi 6 tu ya kuiongoza United. Baada ya hapo, inaaminika kuwa, Ralf Rangnick atakua mshauri wa United kwa miaka 2 ijayo.

Majukumu rasmi ya Rangnick hayajabainishwa na hata yeye mwenyewe, mara kadhaa amekua akisema suala hilo bado hawajalizungumzia na bodi ya United lakini sio tatizo. Licha ya kwamba hajaanza kazi ya ushauri ndani ya klabu, nyuma ya pazia, Ralf Rangnick anafanya kazi yake.

Kuelekea mchezo dhidi ya Liverpool leo usiku, Rangnick ameongelea mambo kadhaa ikiwemo namna ambavyo anadhani uongozi wa Man United unapaswa kuangalia na kushughulikia mambo yanayohusu mpira.

Ralf Rangnick, Ralf Rangnick Anawapasomo United., Meridianbet

Kwa mujibu wa Ralf, kuna pengo kubwa katika namna ambavyo United inaubora na weledi kwenye idara ya matibabu, ufuatiliaji na usajili wa wachezaji. Ametolea mfano wa vilabu kama Liverpool, Man City na Chelsea ambao kwa mujibu wa Ralf, hivi ni vilabu ambavyo vimewekeza kwa watu sahihi na wenye weledi mkubwa kwenye idara hizi.

Pamoja na maboresho ya idara za klabu hiyo, Rangnick pia anaamini zaidi katika kuwekeza kwa watu sahihi, wenye weledi na wanaozijua taaluma zao kinagaubaga. Hawa ni zaidi ya kocha uwanjani. Hakuna kocha duniani mwenye uwezo wa kufanya kazi zote – ndani na nje ya uwanja, hivyo, United wanapaswa kufanya maboresho makubwa kwenye mifumo ya kiutendaji kabla ya kufumua kikosi ambacho pia, kinamapungufu makubwa, mengi yakitokana na mapungufu ya kiutendaji.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa