Kocha wa klabu ya Manchester United Ralf Rangnick amekubali kuwa klabu yake haiwekumaliza kwenye nafasi nne za juu kwa hiyo haitweza kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao.

Kikosi cha Ralf Rangnick kinajianda kumenyana na timu ya Chelsea huku wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza michezo yake miwili iliyopita dhidi ya Liverpool na Arsenal.

Ralf Rangnick
Ralf Rangnick

“Sidhani kama itakuwa na maana sasa kuzungumzia uvumi kuhusu ligi ya mabingwa ulaya, tunahitaji kuwa wakweli,” Alisema Rangnick.

“Hata kama tutashinda michezo yote minne, bado haiko mikoni mwetu. Lakini iko mikononi mwetu kwa jinsi tutakavyocheza, ubora wa kiwango. Hata kwa msimu ujao ni muhimu kumaliza msimu huu kwenye nafasi bora tuwezavyo.”

Alipoulizwa kuhusu madhara ya kutoshiriki ligi ya mabingwa na athari za usajiri kwenye majira ya kiangazi, alisema. “Bila shaka ingekuwa bora ikiwa tutacheza ligi ya mabingwa msimu ujao, lakini pia itaathili klabu nyingine. Hili tatizo halitaathili Manchester United pekee.

“Kuongeza mkataba kwa Bruno kumeonyesha kwanba bado kuna uwezekano wa klabu hii kuvutia wengine na kuja kwa kocha mpya Erik ten Hag. Kuwepo na mfumo mpya na kocha mpya, na aina atakayotaka kucheza, hii bado klabu inayovutia pakubwa.

“Najiandaa kumsaidia kocha mpya na klabu na kila mmoja kwenye klabu, ili kuwafanya vizuri na kubadili mfumo tena kwa msimu ujao ili manchester united kurudi kuwa kwenye klabu za juu.”


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

 

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa