Kocha wa Southampton Ralph Hasenhuttl, amesema mchezo wa leo dhidi ya Manchester United watakuwa na hali ya kujiamini kabla ya mechi ya leo lakini anasisitiza kuwa Saints pia wamejaa imani kufuatia ushindi mara mbili na sare kutoka kwenye mechi tatu za awali.

Alisema: “Siku zote inafurahisha kujipima dhidi ya klabu kama UTD, na kila wakati kuna mazingira maalum ndani ya uwanja kwa mchezo huu.


“Nina uhakika Erik angetiwa moyo sana na jinsi timu yake ilivyocheza dhidi ya Liverpool Jumatatu usiku.

“Kuna vipaji vingi kwenye timu yao na vinaonekana wazi, walionyesha kiwango kizuri cha kuifunga Liverpool, hivyo watakuja hapa wakijiamini leo.

“Vivyo hivyo kwetu sisi, kwa kushinda mara mbili na sare kutoka kwa mechi zetu tatu zilizopita.”


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa