Kiungo wa zamani wa Chelsea na Brazil Ramires ametangaza kustaafu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alikuwa hana klabu tangu alipoondoka Palmeiras mnamo Novemba 2020. Na baada ya muda wa “kutafakari”,.

 

 Ramires Ametangaza Kustaafu

Ramires alijiunga na Joinville kabla ya kujiunga na Cruzeiro, ambapo kiwango chake kilihamia Ulaya na Benfica mnamo 2009 ambapo,  alitumia msimu mmoja tu Ureno kabla ya kupata uhamisho wa pesa nyingi kwenda Chelsea, kwani alifurahia kipindi cha mafanikio zaidi cha maisha yake.

Ramires alikuwa na miaka mitano na nusu Stamford Bridge na alishinda kila kombe la nyumbani mara moja, huku pia akishinda Ligi ya Mabingwa na Ligi ya Europa kabla ya kwenda Jiangsu Suning ya Ligi Kuu ya Uchina.

 

 Ramires Ametangaza Kustaafu

Akitangaza uamuzi wake katika mtandao  kwenye Instagram, alisema: “Baada ya muda wa kutafakari, ningependa kutangaza kwamba nimeamua kumaliza rasmi maisha yangu kama mchezaji wa kulipwa” Alisema.

Ramires alisema kwa wakati huu, anaweza kumshukuru Mungu kwanza, kwani amemuwezesha na kumfikishakatika viwango vya juu zaidi vya michezo.  Pia ameweza kuzishukuru klabu alizopita ambazo ni Palmeiras, Chelsea, Benfica, Cruzeiro, Jiangsu na Joinville na aksema kuwa atazibeba timu hizo moyoni mwake.

Lakini hakuishia hapo tuu alitoa pia shukrani kwa timu ya Taifa ya Brazil kwa kumpa furaha ya kucheza Kombe la Dunia mara mbili, ambayo ilikuwa ni moja ya kutimiza ndoto zake. “Ninashukuru pia kwa wachezaji wenzangu, wafanyikazi, makocha na wasimamizi ambao nilipata furaha kufanya kazi nao”.

 

 Ramires Ametangaza Kustaafu

Ramires alitoa shukurani kwa familia yake mama, watoto, kaka na marafiki wa kweli kwa kuwa upande wake bila masharti kwa miaka yote hiyo, kwa kusherehekea kila mafanikio yake kwamba ni ya kwao ambapo familia na ndugu wamekuwa ni nguvu na motisha kwake.

“Nitaenda pande zingine, lakini kwa furaha na ujasiri uleule niliokuwa nao tangu nilipokuwa mtoto, wakati, kinyume na matarajio yote, niliacha jiji langu ndani ya Rio de Janeiro ili kuona Ulimwengu. Asante kwa kila kitu, mpira wa miguu!”

 

 Ramires Ametangaza Kustaafu

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa