Nahodha wa Real Madrid – Sergio Ramos kukosekana kwenye mchezo dhidi ya Sevilla wikiendi hii.

Ramos alipata majeruhi ya paja mwezi Novemba alipokuwa na timu ya Taifa ya Hispania. Licha ya kurejea mazoezini na kikosi cha Real Madrid, kocha – Zinedine Zidane alisema nahodha huyo atasafiri na kikosi hicho kama tu – atakuwa vizuri zaidi kucheza.

“Hatutafanya maamuzi ya kubahatisha kwa Sergio Ramos. Sitaki kumchezesha mchezaji mwenye tatizo na mwisho wa siku nimuongee tatizo. Tunahitaji wachezaji wote warejee kwenye hali zao.” alisema Zidane.

Ramos, Ramos Kukosekana Kwenye Kikosi cha Madrid, Meridianbet
Sergio Ramos akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuumia akiwa na timu ya Taifa ya Hispania.

Madrid wametoka sare na Villareal (1-1) na kupoteza mchezo dhidi ya Alaves (2-1) ikiwa ni michezo miwili waliyocheza bila uwepo wa Sergio.

Kwenye Ligi ya Mabingwa, Madrid walishinda ugenini kwa Inter (2-0) na kupoteza mchezo dhidi ya Shakhtar Donetsk (2-0) matokeo ambayo yanaweka uwiano wa kufuzu hatua ya mtoano kwa timu za kundi B.

Madrid wanashika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa La Liga wakiwa na pointi 17. Wamezidiwa pointi 7 na vinara wa msimamo wa ligi hiyo – Real Sociedad na wameachwa pointi 6 na Atletico Madrid ambao watakutana wikiendi ijayo.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Ramos, Ramos Kukosekana Kwenye Kikosi cha Madrid, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

22 MAONI

  1. Real haijasajiri wachezaji wa viwango vya kimataifa, kocha anatumia uzoefu na kuingiza ingizo jipya kutoka kikosi B na kwabahati mbaya bado mambo ni magumu. Umekuwa msimu mgumu zaidi hasa baada kuumia kwa Ramos, Hazard, kuondoka kwa Bale na kibaya zaidi beki ya kushoto kucheza kwa kiwango hafifu mno

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa