RAMOVIC AWATAKA WACHEZAJI YANGA KUPAMBANA

SAED Ramovic, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa ni lazima wachezaji waendelee kupambana kwenye mech izote ili kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja.

Yanga kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa uliwakosa wachezaji watatu ambao hawakuwa fiti ni Ladack Boka, Khalid Aucho na Clement Mzize.RAMOVICMwisho mchezo huo wa pili kwa mrithi mikoba ya Miguel Gamondi ubao ulisoma Namungo 0-2 Yanga kwa mabao ya Kennedy Musonda na Pacome.

 

Kocha Ramovic huyo amesema kuwa kuna ushindani mkubwa kwenye mechi ambazo wanacheza jambo ambalo linawafanya wawe kwenye maandalizi kila wakati.

“Tuna kikosi kikubwa cha wachezaji 25 mpaka 26 tunatakiwa kuwa kwenye ubora mkubwa ndani ya uwanja na tunaamini tutafanya vizuri licha ya ushindani ambao upo.

“Jambo la msingi ni kwa wachezaji kujituma muda wote kusaka matokeo na inawezekana kuwa kwenye mwendelezo bora kila kitu kitakuwa sawa.”Alisema Ramovic

Acha ujumbe