Siku za golikipa wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Uingereza Aaron Ramsdale zinahesabika ndani ya klabu hiyo kwa kile kinachoelezwa kutokua na furaha ndani ya timu hiyo.
Ramsdale ambaye alikua golikipa namba moja ndani ya timu hiyo lakini mambo yamebadilika baada ya usajili wa golikipa David Raya ambaye ndio amekua golikipa namba moja ndani ya Arsenal.Baba mzazi wa golikipa huyo amefanya mahojiano na kituo kimoja nchini Uingereza na kusema mwanae hana furaha ndani ya klabu hiyo na ni ngumu kumuona kijana wake amepoteza furaha ndani ya klabu hiyo.
Baba mzazi wa mchezaji alisema pia golikipa huyo ataendelea kupambania mataji ndani ya Arsenal, Lakini alienda mbali zaidi na kusema David Raya ni golikipa mzuri na kuchukua namba ya mwanae sio kosa lake.Kauli ya Baba mzazi wa golikipa Aaron Ramsdale inaonesha kua mchezaji huyo hana furaha ndani ya timu hiyo na ni wazi hataki kua golikipa namba mbili, Hivo njia pekee ya kuhakikisha anapata muda wa kucheza zaidi ni kuondoka ndani ya klabu ya Arsenal.