Klabu ya Rangers ya nchini Scotland imetawazwa mabingwa wa ligi hiyo (Scottish Premiership Champions) baada ya mahasimu wao Celtic kushindwa kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Dundee United siku ya jana.
Steven Gerrard aliiongoza timu hiyo kuwafunga 3-0 St Mirren katika uwanja wa Ibrox siku ya jumamosi na kubaki kuwa timu ambayo haijafungwa mpaka sasa katika ligi hiyo msimu huu.

Rangers wamecheza michezo 32 mpaka sasa wakiwa na alama 88 wameshinda michezo 28 sare 4 huku wakiwa wamefunga magoli 77 na kufungwa 9.
Alama hizo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote katika ligi hiyo ikiwa imebaki michezo 6. Celtic aliye nafasi ya pili amecheza michezo sawa na Rangers akiwa na alama 68 akishinda 20 sare 8 na kupoteza 4.
Huo ni taji la kwanza kwa Steven Gerrard kama kocha baada ya kuchukua nafasi ya Govan katika majira ya kiangazi mwaka 2018.
Hongera yao rangers
Safi
Safii sana
Vizuri
Safi
Safii
Wametishaa sana
Safii