Rangnick Atetea Uamuzi wa Kumtoa Ronaldo.

 

Meneja wa muda wa Manchester United, Ralf Rangnick ametetea uamuzi wake wa kumtoa Cristiano Ronaldo baada ya mchezaji huyo kutoridhishwa katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Brentford.

 

Magoli ya United yalifungwa katika kipindi cha pili kupitia kwa Anthony Elanga, Mason greenwood na Marcus Rashford na kurejesha matumaini ya kurejea nne bora katika ligi ya primia.

“Ni kawaida, mshambuliaji kutaka kufunga,” Rangnick aliiambia BT Sports. “Lakini amerudi kutoka kwenye majeraha na tunapaswa kukumbuka kuna michezo mingine inakuja.

“Pia kwa kile kilichotokea Villa Park tulipaswa kulinda ushindi leo na ni muhimu tulirudi katika mfumo wa mabeki watano na tunavyoshindwa kuzuia kutofungwa tunapaswa kuhakikisha hakuna kingine kitatokea.

“Mwitikio niliouona ni, ‘Kwanini mimi? Kwanini umenitoa mimi?’ Nilitakiwa nichukue maamuzi kwaajili ya faida ya timu na klabu. Nilifanya hivyo hata tulipoongoza 2-0 Villa park na sikutaka kurudia makosa kama yale tena.” aliongeza Rangnick.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe