Rangnick Ni Mpini Au Makali Kule United?

Kuna vilabu vya soka, halafu kuna Manchester United. Huku kuna soka na biashara. Ralf Rangnick ni mpini au makali?

Akiwa amekabidhiwa kazi ya kuiongoza Man United kwa miezi 6 pekee, Ralf Rangnick anakazi ya ziada kuelekea mwishoni mwa msimu huu. Matokeo uwanjani bado ni changamoto kwa The Red Devils. Vipi sokoni? Ralf analolote?

Hakika, kufanya kazi Manchester United ni kama ule wimbo wa Goya Menor – Ameno Amapiano (“You wanna chill with the big boys”). Unaweza kuwa sehemu sahihi au kwenye kichaka kizito kutoka. Yote yanawezekana ndani ya United.

Jose Mourinho, aliipatia United mataji 3 licha ya kutokuwa na nguvu kubwa ya kufanya maamuzi hasa kwenye soko la usajili.

Hakuna muunganiko thabiti kati ya wachezaji, benchi la ufundi, uongozi wa timu (bodi) na wamiliki. Kwa sehemu kubwa, huwezi kujua nani ni mpini na nani ni makali. Ama hakika, Jose Mourinho anaweza kuwa shuhuda wa hili.

Kila kocha aliyepita United baada ya Sir Alex Ferguson, alikutana na rabsha za aina yake. Kuna waliobahatika kuwa upande wa makali (David Moyes, Lois Van Gaal na Ole Gunnar Solskjaer) na wengine, ni mipini tu (Jose Mourinho).

Van Gaal (kushoto) na Moyes (kulia), waliaminiwa na uongozi wa United kwa vipindi tofauti. Walipewa nguvu kwenye soko la usajili lakini, walishindwa kuboresha kikosi chenye ushindani kwenye EPL na Barani Ulaya. Wote wawili waliishia kufukuzwa kazi.

Sasa hivi ni zamu ya Ralf Rangnick, yeye anasimama wapi katika hili? Dirisha la usajili lipo wazi kwa muda sasa. Kiuhalisia, United wanahitaji kusajili kiungo mkabaji kama wanampango wa kuinusuru nafasi yao ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Ralf huwenda akawa anajua anachokitaka ndani ya United lakini, anamakali ya kuhakikisha matakwa yake yanatimia au, kazi yake ni kuongoza timu kama ilivyo na hana makali yeyote kwenye upande wa kufanya maamuzi sokoni?

Ole Gunnar Solskjaer aliminiwa na kupewa nguvu kubwa na bodi ya wakurugenzi wa Man United. Matokeo uwanjani, yalimfukuzisha kazi na timu kuchukuliwa na Ralf Rangnick kama kocha wa muda.

Kuna kila dalili kuwa, licha ya Ralf kuhitaji kuboresha kikosi chake majira haya ya baridi, vigogo wa Manchester United, hawana mpango wa kumtengea fungu lolote kocha huyu ambaye, ni kocha wa muda tu na hivyo, makali yao watayaweka kwa kocha mpya atakayepatikana baada ya msimu huu.

Ralf, muasisi wa gengenpress, amua mwenyewe – unazika au unasafirisha? Huu msala wa Manchester United utakuangukia mwishoni mwa msimu. Hii ndio Manchester United, inakuvutia, unajiunga nayo ila, utayoyakuta ndani ni vita – nani mpini, nani makali? Jembe ni Man United.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe