Kocha wa muda wa klabu ya Manchester United Ralf Rangnick anasema kuwa hajafurahishwa na kiwango cha walinzi wake kwenye mchezo wa dhidi Norwich na amesema itakuwa ni bahati kuondoka na alama moja kwa ulinzi ule.

Ijapokuwa klabu ya Manchester United imefanikiwa kupata alama tatu kwenye mchezo wa jana, huku Ronaldo akifanikiwa kufunga magoli matatu peke yake na kufikisha hat-trick ya 60 kwenye maisha yake ya soka mpaka sasa, lakini pia kikosi cha Rangnick kiliruhusu magoli mawili ya kizembe sana.

Rangnick

Rangnick ameikosoa safu yake ya ulinzi kwa kurusu goli mbili dhidi ya Norwich kwenye mchezo wa jumamosi huku akinukuliwa akisema, “hakuna timu yoyote ya ligi kuu inaweza kutoa zawadi ya kama ile.

“Kila mmoja ameona mchezo wa leo na kila mmoja anafahamu aina ya timu tunayokwenda kucheza nayo siku ya jumanne. Liverpool amemfunga Man City, majogoo wapo fainali na wananafasi ya kuweza kushinda makombe manne msimu huu.

“Kama tukicheza kama tulivyo cheza leo, itakuwa ngumu kupata hata alama moja. Hivyo ndivyo tunapaswa kuwa wa wazi, inapaswa tuwe makini timu pinzani wanapokuwa na mpira.” Alisema Rangnick


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa