Kocha wa muda wa Manchester United, Ralf Rangnick amekielezea kitendo cha Liverpool kuifunga timu yake goli 4-0 katika Mchezo wa EPL kwenye Uwanja wa Anfield kuwa ni cha aibu na fedheha.
Akizungumza baada ya mchezo amesema wataijenga upya timu hiyo na huenda katika kipindi kijacho cha usajili wakanunua wachezaji wapya 10 ili kuimarisha timu.
Manchester United ilifungwa goli 5-0 katika mchezo wa awali uliochezwa Old Trafford, kwa msimu timu hiyo imefungwa jumla ya goli 9-0 na Liverpool na Rangnick anasema anaiona timu yake ikiwa nyuma ya vijana wa Jurgen Klopp kwa miaka 6.
Rangnick anatarajiwa kuwa mshauri wa klabu hiyo kuanzia msimu ujao baada ya United kupata kocha wa kudumu, huku kocha wa Ajax, Ten Hag akitajwa kuchukua mikoba hiyo.
Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.