Rapa Aitch Afichua Jezi Mpya ya United Kabla ya Kuzinduliwa Rasmi

Rapa wa Uingereza Aitch amefichua jezi mpya ya Manchester United ya nyumbani kwa ajili ya kampeni ya 2023-34 huko Glastonbury jana siku chache kabla ya kuzinduliwa rasmi.

 

Rapa Aitch Afichua Jezi Mpya ya United Kabla ya Kuzinduliwa Rasmi

Jezi za adidas zikitarajiwa kuonyeshwa Jumanne, shabiki huyo wa zamani wa United jina halisi Harrison James Armstrong aliwapa mashabiki picha kamili ya jezi hiyo walipokuwa wakitumbuiza kwenye tamasha la muziki.

Aitch alivalia jezi mpya ya Manchester United alipokuwa akiwaburudisha maelfu ya mashabiki wa muziki huo.

Rapa Aitch Afichua Jezi Mpya ya United Kabla ya Kuzinduliwa Rasmi

Machester United ambayo ipo chini ya Ten Hag wanaendelea kujifua kwaajili ya msimu ujao huku dili lao la kumsajili kiungo wa Chelsea Mason Mount likipigwa chini kwa mara ya tatu.

Mchezaji huyo ameonyesha nia ya kujiunga na United ambao mechi yao ya kwanza ya msimu wa 2023/24 wataanza dhidi ya Wolveshampton.

 
Community Verified icon

Acha ujumbe