Nyota wa Manchester United Marcus Rashford anaamini kuwa klabu yake sasa imerejea kwenye fomu chini ya Ole Gunnar Solskjaer baada ya kuyumba yumba kidogo kwa misimu kadhaa.
Nyota huyu anadai kuwa kikosi cha sasa kipo vizuri zaidi ukifananisha kikosi hicho miezi 12 iliyopita wakiwa chini ya Jose Mourinho.
United wanaanza kampeni yao ya msimu wa 2019/20 wakiwa na gemu ngumu dhidi ya Chelsea, mechi ambayo ni ya kwanza ya EPL kwa Frank Lampard akiwa kama meneja kwa Chelsea.
Rashford licha ya kutambua umuhimu wa Ole Gunnar na Mourinho, wote kwa pamoja, anasema kuwa kawaida utajifunza vitu tofauti kwa mameneja tofauti.
Akianza kwa kumzungumzia Van Gaal, anamtaja kuwa meneja huyu alikuwa ana subira na alimpa mda wa kujifunza. Hakuwa akimjaza vitu vingi kwa pamoja katika mafundisho yake.
Kwa upande wa Mourindo, anaona yeye pamoja na wenzake kikosini walipata nafasi ya kujifunza soka zaidi hasa katika kipengele cha ulinzi.
Akimtofautisha Ole Gunnar na watangulizi wake wa juu, anasema kipindi hiki wanajaribu kufanya yote kwa pamoja kwa kuwa Ole anaifahamu vyema klabu.
Kwa sasa anaamini klabu imetulia baada ya kuwa katika misukosuko ya kutofanya vizuri. Kwa upande wake haoni wa kumtupia lawama moja kwa moja kama ni uongozi, meneja au wachezaji, anaamini walipo wanaweza kusonga mbele na kufanya viziuri.
Lydia Emmanuel Magoti
Rashford yupo sahii kwanacho kiongea kajisemeha yeye Kama yeye