Rashford Kuanza Dhidi ya Liverpool

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Marcus Rashford amerejea kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo dhidi ya Liverpool leo baada ya kuanzia kwenye mchezo dhidi ya Chelsea.

Rashford alianzia nje katika mchezo ambao Man United walipoteza dhidi ya Chelsea kwa mabao manne kwa matatu, Lakini leo ameonekana kwenye kikosi kilichotaka kua ataanza mchezo huo mkali kabisa utakaopigwa jioni hii.rashfordMshambuliaji huyo amekua hana mwendelezo mzuri wa ndani ya kikosi hicho msimu huu kwani hata namba zake zinaonesha ukilinganisha na msimu uliomalizika, Hii ikichangia hata kocha wake Erik Ten Hag kumpumzisha.

Mshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Uingereza licha ya kutokua na msimu mzuri lakini amekua moja ya wachezaji wenye takwimu nzuri sana dhidi ya klabu ya Liverpool, Mshambuliaji huyo mpaka sasa amefunga mabao saba dhidi ya Majogoo hao wa Anfield hivo ni wazi amekua mwiba mchungu kwao.rashfordKuanza kwa mshambuliaji Marcus Rashford leo dhidi ya Liverpool ni wazi kocha Erik Ten Hag ataendelea na mfumo wake wa 4-3-3, Ambapo safu yake ya ushambuliaji itaundwa na staa huyo wa kimataifa wa Uingereza, Rasmus Hojlund, na kijana mdogo Alejandro Garnacho.

Acha ujumbe